- Tunapozungumzia ROHO MTAKATIFU haimaanishi kuwa ni nguvu fulani, bali kama Nafsi ya tatu ya Mungu. Ni muhimu kuelewa kuwa MUngu ni mmoja katika Nafsi tatu,hutofautiana katika utendaji kazi wao 1 yohana 5:7-8; 2 wakorintho 3:17-18.
- ROHO MTAKATIFU anao umuhimu mkubwa sana katika kanisa kwani ndiye uhai wa kanisa. Kinachotofautisha kanisa hai la Mungu na makanisa mengine ni namana wanavyompa nafasi ROHO MTAKATIFU.IKumbukwe kuwa kanisa la rohoni lilianzishwa mara tu ya kushuka kwa ROHO MTAKTIFU MATENDO 1:8; 2:1-4
- Hata kwa mtu binafsi kiwango unachomruhusu kutenda kazi ndani yako, ndicho kiwango ambacho anahuisha maisha yako. Hivyo basi ni muhimu kutambua/ kuelewa umuhimu wa ROHO MTAKATIFU KWA KANISA NA KWA MAISHA YA MAISHA BINAFSI.
- Umuhimu wake unatokana na kazi anazozifanya kwa kanisa na mtu binafsi.
- ROHO MTAKATIFU HUMFANYA MTU KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.
- Roho Mtakatifu kwa asili yake ni msafi wala hachangamani na uchafu , Hivyo basi ana kawaida ya kuzalisha vitu vitakatifu ndani ya mtu. . LUKA 1:34-35 Biblia inasema "Malaika akajibu akamwambia, ROho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu za aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu"
- Roho Mtakatifu pia hujishulisha na kuondoa dhambi ndani ya kanisa na mtu binasfi; Tabia hii ya Roho mtakatifu kujishughulisha na dhambi ilidhihirika wazi katika kitabu cha matendo ya mitume wakati wa kanisa la kwanza. Anania alipojaribu kuleta wizi ndani ya kanisa Roho mtakatifu mwenyew alishughulika kumwadhibu. kumbuka kwamba wakati huo ndio tu alikuwa amezinduliwa, hivyo alikuwa na nguvu kamili ndani ya kanisa. (MATENDO 5:1-5.)
- Roho mtakatifu ndiye mhusika mkuu wa karama hizo. karama zipo za aina mbalimbali "lakini kazi hizi zotehuzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawiakila mtu peke yake kama apendavyo yeye" 1 WAKORINTHO 12:11.
- Yesu hutoa huduma tano ndani ya kanisa lakini huduma bila ROHO MTAKATIFU huduma hiyo haitakuwa na ufanisi, na inawezekana isiwaguse watu. Na hii ndiyo inayowatofautisha watumishi wa Mungu, kila mmoja anatofautiana na mtumishi mwingine katika karama na hii hutolewa na Roho mtakatifu mwenyewe kama apendavvyo, pamoja na hilo ni kusudi la kulijenga kanisa " Basi ninyi mmekuwa mwili wa kristo, na viungo kila mmoja pee yake"(1 KOR 12:27)
- Katika kitabu cha 1 SAMWEL 17:38 -50, TUNAJIFUNZA JAMBO LA MUHIMU KUHUSU ROHO MTAKATIFU. Ni hadithi inayomhusu kijana Daudi, Ili kumuua Goliathi alikuwa mambo yafuatayo.
ii.Fimbo - kwa maana ya neno la Mungu.
iii. Kombeo - kwa maana ya Roho Mtakatifu.
iv. Mawe matano - huduma tano.
v. jina la Bwana - jina la Yesu.
- Daudi alikuwa mchunga kondoo , alichagua jiwe(huduma) la kichungaji na kutumia kombeo (nguvu ya Roho Mtakatifu) kumpiga Goliathi kwa jina la Bwana (jina la Yesu) ndipo akamshinda ushindi mkuu.
- Hii inatuonesha umuhimu kuwa na Roho Mtakatifu ili kuzidi kuchochea huduma na karama zilizo ndani yako. 1 TIMOTHEO 4:14 " Usiache kutumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee"
3.ROHO MTAKATIFU HUMFANYA MTU AU KANISA KUWA NA IBADA YA BUBUBJIKO NA KUZAMA KWA NDANI, NA KUONDOA UKAME WA KIROHO, KWA KUZIFANYA IBADA KUWA HAI. EZEKIEL 37: 1-14
- Ili ibada iwe hai inategemeana na kiwango cha ujazo wa Roho Mtakatifu katika ibada, hii ina maana kuwa hata nguvu za Roho Mtakatifu katika kanisa ama mtu mwe nyewe hutegemea kiwango cha ujazo wa Roho ndani yake.
- katika ujazo wa Roho Mtakatifu kuna viwango vinne vya ujazo wa Roho Mtakatifu kama vile biblia inavyotufundisha katika kitabu cha EZEKIEL 41:1-10.
ii.kiwango cha pili - magotini (ujazo wa kawaida)
iii.kiwango cha tatu - viunoni ( ujazo wa wengi walionao)
iv.Kiwango cha nne - Mwili mzima (kiwango kinachotakiwa kwa wakati tulio nao)
- Roho Mtakatifu anapaswa kutujaa kila siku, maana ndiye pia anabebe neema ya maombi (LUKA 11:9-13; ZEKARIA 12:10)
- Neno msaidizi haina maana ya mtumwa au mfanyakazi.Roho Mtakatifu ana kazi ya kutusaidia pale tunapohitaji msaada, kama vile katika maombi nk. (WARUMI 8:26; YOHANA 14:26)
- Wenye kazi ya kuomba sio sisi, tunapomruhuusu Roho Mtakatifu yeye hutusaidia kuomba kwa mapenzi ya MUNGU.( YUDA 1:28-29; 1 YOHANA 5:14-15; WARUMI 8:26)
- Roho Mtakatifu kama MSAIDIZI atafanya mambo yafuatayo kwa mwamini;
- Roho Mtakatifu atamuongoza katika KWELI, Hivyo nam yeye kuwa mwalimu wa hiyo kweli. YOHANA 14:16-17;25-26.
- Atawaongoza Watumishi wa Mungu kuhubiri kweli ya Neno la Mungu na kuwaambia watu makosa yao. 1 WAKORINTHO 2:10 -14.
- Roho Mtakatifu atawahuisha watu kwa kumpa nafasi ya kwanza katika kutenda ili awafikishe katika kimo cha utimilifu wa kristo. WARUMI 8;9-17; WAGALATIA 5:16-17.
- Roho Mtakatifu atazalisha tunda la Roho ndani ya mtu aliyempa nafasi kama msaidizi na mwalimu WAGALATIA 5:22-23.
- Roho Mtakatifu kama msaidizi atawajulisha watu wake mafumbo ya Mungu (DANIEL 2:20-23; matahayo 15;26; 1 wakorintho 2:10-16)
5. ROHO MTAKATIFU HUMFANYA MTU ASICHOKE WOKOVU- MATENDO 1:8 - Mtu asiye na Roho Mtakatifu atachoka haraka katika kuendelea na wokovu, hii ni kwa sababu ya kushinmdwa kutoa nafasi ya kuongozwa na Roho mtakatifu. ISAYA 40:28-31; WAEBRANA 2:1-4.
- Petro kabla hajajazwa Roho Mtakatifu alimkana Yesu mbele ya watesaji , lakini baada ya kujazwa Roho Mtakatifu yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtangaza siku ya pentekoste LUKA 22:54-61; MATENDO 2;14.
- Hata kama unapitia magumu ya aina gani yeye atakutia nguvu ya kuvumilia na hatimaye jawabu la magumu hayo kupatikana kwa maana " jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamojana lile jaribu atafanya na mlangowa kutokea ili mweze kustahimili. 1 WAKORINTHO 10:13.
- Roho mtakatifu kama mafuta, moto hufanya kazi ya kuvunja vifungo vilivyowafunga watu katika maeneo mbalimbali ZABURI 97:3; WAEBRANIA 12:29.
- Mhuri ni alama maalum inayotumika kutambulisha kitu fulani, na kuonyesha umliki wa halali wa kitu hicho.Hivyo basi Roho Mtakatifu kama mhuri wa Mungu hutumika kuonyesha umiliki halali wa Mungu kwako, unapojazwa Roho mtakatifu ndipo unamilikiwa na Mungu. UFUNUO 7:2-3; 9:4; EZEKIEL 9:4,6.
- Kanisa au mtu hutambuliwa na Mungu kama mali yake kutokana na muhuri wake ambao ni ROHO MTAKTIFU. WAEFESO 1;13-14, 4:30; WARUMI 8:9.
- Kama Roho Mtakatifu ni muhuri, basi yeye ndiye arabuni ya urithi wetu. (WAEFESO 1:13-14; 2 WAKORINTHO 1:21- 22; 5:5.
ROHO MTAKATIFU KAMA ARABUNI KATIKA UNYAKUO WA KANISA.
- Yesu kristo alitufundisha katika habari za unyakuo utakaotokana na ujio wake wa mara ya pili,namn itakavyokuwa katika kanisa MATHAYO 24:29-31.
- Lakini pia, hukumu inapaswakuanzia katika nyumba ya Mungu yaani kanisa,maana yake nini kuna watu ambao hawatahusika katika unyakuo ingawa wameokoka
- katika unyakuo wa kanisa wale tu walio na Roho Mtakatifu ndio watakaonyakuliwa. Roho Mtakatifu atakuwa kama sumaku ndani yao, naye Yesu angani atakuwa kama chuma,kwa hiyo uwezo sumaku ndio uwezo wa kunaswa na chuma kwa umbali fulani.
- Ni muhimu kuzingatia kuwa unaweza kuwa na wokovu, lakini hauwezi kuingia mbinguni kama hauna dhamana(arabuni) MATHAYO 25:1-12 MWISHO.MUNGU AKUBARIKI SANA
No comments:
Post a Comment